Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa
Stars’ itaweka kambi Afrika Kusini kujiandaa na
mchezo wa raundi ya pili wa kutafuta tiketi ya
kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2018 dhidi ya
Algeria, mwezi ujao.
Awali Stars ilipanga kuweka kambi nchini Misri,
lakini Shirikisho la Soka nchini (TFF) na benchi la
ufundi la Stars chini ya kocha, Boniface Mkwassa
walilazimika kupangua ratiba hiyo kwa kuhofia
kuwa jirani na wapinzani wao.
Kwa mujibu wa kiongozi mmoja mkubwa wa TFF,
alidai kuwa uamuzi uliofikiwa ni Stars kwenda
Afrika Kusini ambapo kocha Mkwassa
amependekeza timu hiyo ikae kambini kwa siku
10 kuanzia Novemba 3 kujiweka tayari kwa
mchezo huo utakaopigwa Novemba 14, Dar es
Salaam.
“Kutokana na kambi hiyo, ratiba ya mechi kwa
timu za Simba, Yanga na Azam ambazo
zilipangwa kucheza mwishoni mwa mwezi huu
sasa zitasogezwa mbele ili kuwapa fursa
wachezaji wa Stars kujiandaa vyema na mchezo
huo,” kilieleza chanzo chetu.
Mechi za ligi ambazo zitasogezwa kupisha
maandalizi ya Stars ni ile ya Simba na Majimaji,
Kagera Sugar dhidi ya Yanga na Azam FC dhidi
ya Toto Africans. “Tunaijua Algeria ni timu imara
na inayokamata namba moja katika viwango vya
ubora Afrika. Pia ina uzoefu kwenye Kombe la
dunia, hivyo tunapaswa kujiandaa kikamilifu ili
kuikabili kwani lengo ni kufuzu kwa hatua ya
makundi,” alisema mtoa habari huyo ambaye ni
miongoni mwa viongozi waandamizi wa TFF
hakupenda kutajwa jina lake.
Alifafanua kwamba, benchi la ufundi la Stars
limeamua kuendelea kuwa na kikosi kilichoiondoa
Malawi katika mchezo wa awali na ndicho hicho
hicho kitakachokwenda kuweka kambi nchini
Afrika Kusini.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi alipoulizwa juu ya
kambi hiyo alisema watajadiliana na benchi la
ufundi na Katibu Mkuu Celestine Mwesigwa
atatoa taarifa rasmi.
“Muda huu niko katika kikao na katibu mkuu na
mratibu wa timu ya Taifa Ahmed Mgoyi, tupe
muda tutakujibu juu ya kambi hiyo,” alisema
Malinzi pasipo kukanusha wala kukubali kikosi
hicho kwenda Afrika Kusini.
Asante kwa kutembelea Hope FM Iringa, Asante kwaku-share habari hii, Kama una Maoni, Ushauri, Story ya ku-share na sisi na au Unahitaji msaada...!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni