Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



The Wikiendi ijayo Sam Allardyce atakuwa kocha wa kwanza kufundisha vilabu viwili pinzani vya Sunderland na Newcastle, wakati atakapoiongoza rasmi kama kocha klabu ambayo kawahi kuichezea zamani katika mchezo wa ligi kuu ya England. 
Alladyce na anaungana na wachezaji kadhaa ambao wameshaeahi kuingia kwenye rekodi ya kuvitumikia vilabu pinzani vya ligi moja kwa wakati tofauti – huku Big Sam akiwa kama kocha sasa tuangalie wachezaji wengine wanaounda kikosi chake cha wachezaji waliowahi kuvitumikia vilabu pinzani vya ligi moja kwa wakati tofauti.
        
Golikipa: Petr Cech
Chelsea 2004-15, Arsenal 2015-…..
Hakukuwa na hisia mbaya katika uhamisho wa Petr Cech kwenda Gunners – baada ya golikipa huyo kuitumikia Chelsea kwa miaka 9 kwa mafanikio makubwa. Lakini chaguo lake la klabu mpya lileta mshangao. Kwa kadri siku za kukaa nje ya uwanja kwa Thibaut Courtois zinavyozido kwenda ndivyo mashabiki wa The Blues watakavyokuwa wakichukizwa na Cech kwenda wapinzani wao ambao mpaka sasa wapo juu yao katika msimamo wa ligi.
          
 Beki wa Kulia: Christian Panucci
AC Milan 1993-96, Inter Milan 1999-2001

Beki huyu wa kulia alicheza kwa mafanikio kwa misimu miwili na AC Milan akifanikiwa kushinda Serie A mara mbili na Ubingwa wa ulaya 1994, lakini baadae akaondoka kujiunga na Real Madrid 1997, kabla hajarudi nyumbani mwaka 1999 na kujiunga mahasimu wa jadi ya AC Milan – Inter.
         
Beki wa kati William Gallas
Chelsea 2001-06, Arsenal 2006-10, Tottenham 2010-13

Hakuwa na tatizo lolote kuhama kutoka Chelsea kwenda Arsenal akiwa kama sehemu ya malipo ya Chelsea katika usajili wa Ashley Cole. Chelsea wakatoa taarifa muda mfupi baadae kwamba Gallas alitishia kujifunga magoli mwenyewe ikiwa hatoruhusiwa kujiunga na Arsenal. Arsenal walipogoma kukubaliana na matakwa yake ya mshahara mnamo mwaka 2010, akaamua kujiunga na wapinzani zaidi wa Arsenal – klabu ya Tottenham Hotspur, hivyo kuweka rekodi ya kuvichezea vilabu hivyo vya London.
        
Beki wa kati: Sol Campbell
Tottenham 1992-2001, Arsenal 2001-06, 2010

Kipenzi cha mashabiki wa Spurs aiamua kuacha mpaka mkataba wake ulipoisha, akakataa mkataba mpya ambao ungemfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya Spurs. Akitoa sababu kwamba alitaka kujiunga na klabu inayocheza kwenye Champions League, lakini uhamisho wake wa kwenda Arsenal ulifanywa siri mpaka siku alipotangazwa rasmi na Arsenal – katika mkutano ambao ulikuwa wa kumtangaza golikipa mpya wa Arsenal – Richard Wright. Uhamisho huo umemjengea uhusiano mbaya sana na mashabiki wa Spurs mpaka leo.
       
Beki wa kushoto: Ashley Cole
Arsenal 1998-2006, Chelsea 2006-14

Ofa ndogo mno iliyotolewa na Arsenal ilibaki kidogo imsababishie ajali ya gari Ashely Cole – na huo ndio ukawa mwisho wa mchezaji huyo ndani ya Arsenal. Aliondoka kutoka kaskazini mwa London na kwenda magharibi mwa jijihilo kujiunga na kikosi cha Jose Mourinho. Mashabiki wa Arsenal mpaka leo wanamuita mchezaji huyo – Cashley Cole.
        
Winga wa kulia: Luis Figo
Barcelona 1995-2000, Real Madrid 2000-05
Mreno huyo inawezekana anachukiwa zaidi na mashabiki wa FC Barcelona a walilithibitisha hilo walipomtupia kichwa cha nguruwe uwanjani. Real walilipa kisi cha paundi million 31 na kuvunja mkataba wa Figo kutoka Barca kwenda Real – usajili huu ndio ukawa aa kwanza katika kuunda kikosi cha Magalactico.
 
Kiungo wa kati: Patrick Vieira

AC Milan 1995, Inter Milan 2006-10
Mshindi wa Kombe la dunia alijiunga na AC Milan akitokea Cannes mwaka 1996, lakini aliamua kutojali mashabiki timu wangekuwa na hisia gani juu wakati Inter Milan alipoamua kumchukua kutoka Juventus iliyoshushwa daraja 2006.
        
Kiungo mshambuliaji: Michael Laudrup

Barcelona 1989-94, Real Madrid 1994-96

Moja ya viungo bora kabisa kuwahi kucheza soka barani ulaya, mdenishi huyo alijiunga na kikosi cha Johan Cruyff ndani Barcelona 1989, akashinda La Liga mara 4 na kombe la European Cup 1992. Alipogombana na Cruyff akaamua kuondoka na akajiunga na Real Madrid.
       
Winga wa kushoto Peter Beardsley
Liverpool 1987-91, Everton 1991-93

Alijiunga na Liverpool kutoka Newcastle mwaka 1987 baada ha Kenny Dalglish kuamua kuacha kucheza soka na kurudi kufundisha. Mchezaji huyo baadae akaamua kujiunga na Everton mwaka 1991 baada ya kuja kwa Dean Saunders katika klabu ya Liverpool, alitumia miaka miwili kuitumikia Everton na kuingia kwenye rekodi ya kufunga magoli kwa timu zote mbili katika mchezo wa Merseyside derby. Beardlsey pia amewahi kuitumikia Manchester United alipokuwa kinda.
       
Mshambuliaji: Ronaldo

Barcelona 1996-97, Inter Milan 1997-2002, Real Madrid 2002-07, AC Milan 2007-08
Ronaldo De Lima aliingia kwenye matatizo wakati anajadiliana mkataba mpya na Barcelona mwaka 1997. Inter wakajitosa na kuamua kuvunja rekodi ya dunia ya wakati huo kwa kulipa kiasi cha £19.5m. Akawakera zaidi aliporejea Spain na kujiunga na Real Madrid iliyokuwa imejaa wachezaji kama akina Figo na Zidane, Figo. Baada ya Madrid Robaldo akarudi Italia na kwenda kujiunga na AC Milan
        
Mshambuliaji: Zlatan Ibrahimovic

Inter Milan 2006-09, AC Milan 2010-12

Mshambuliaji huyo wa KiSwedish mwenye kujiona kwelikweli, alishinda ubingwa wa Serie A akiwa na Inter Milan kwa miaka 3 mfulilizo. Alirudi nchini Italia kwa mkopo na kuitumikia AC Milan baada ya kutoka FC Barcelona. Zlatan aliwakera sana mashabiki wa Inter. – hata hivyo Zlatan ndio mshambuliaji pekee baada ya Ronaldo De Lima kuwahi kuzifungia magoli timu zote katika vipjndi viwili tofauti katika mchezo wa Milan Derby.


Chapisha Maoni