Timu ya taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15)
imeingia kambini jana jioni katika hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es
salaam, kujiandaa na ziara ya mafunzo katika ukanda wa Afrika Mashariki
itakayoanza Disemba Mosi mwaka huu.
Kocha wa timu hiyo Sebastian Mkomwa amesema vijana wote
wameshawasili jijini Dar es salaam na leo wameanza mazoezi asubuhi katika
uwanja wa Karume watakapokua wanajifua kila asubuhi na jioni mpaka siku ya
safari.
Kikosi
cha wachezaji 24 kimeingia kambini kujifua na ziara ya Afrika Mashariki, ambapo
timu hiyo inaandaliwa kwa ajili ya kushiriki kuwania kufuzu kwa fainali za
Mataifa Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, zitakazofanyika mwaka
2017 nchini Madagascar.
Timu
ya Taifa ya vijana imeakua na program ya kukutana kila mwisho wa mwezi kwa
ajili ya kufanya mazoezi na kucheza michezo ya kirafiki na timu za kombani za
U15 katika mikoa mbalimbali nchini, ambapo kwe mwezi Disemba itakua pamoja kwa
wiki tatu katika nchi za Afrika Mashariki ikicheza michezo ya kirafiki.
Disemba
Mosi, U-15 itasasiri kuelekea jijini Mwanza ambapo itacheza mchezo mmoja wa
kirafiki na kombani ya jijini Mwanza (U17), kasha kusafiri kueleka mkoani
Kigoma itakapocheza michezo miwili dhidi ya kombaini ya mkoa wa Kigoma (U17) na
timu ya Taifa ya Burundi (U17).
Ziara
hiyo itaendelea katika jiji la Kigali kwa kucheza michezo miwili dhidi ya timu
ya Taifa ya Rwanda (U17), Jinja dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda (U17), Nairobi
dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya (U17) na kumalizia kwa mchezo dhidi ya kombaini
ya mkoa wa Arusha (U17) na kurudi jijini Dar es salaam.
Chapisha Maoni