Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa
timu 24 za makundi A, B, C na D kucheza katika viwanja 12 mbalimbali
nchini, kusaka nafasi nne za kupanda Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao (StarTime
First League).
Kesho Jumamosi Kundi A, Mvuvuma FC watakua wenyeji wa Abajalo FC
ya Tabora uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, Transit Camp watacheza
dhidi ya Mirambo FC uwanja wa Kamabarage Shinyanga, huku Singida United
watawakaribisha Green Warriors katika uwanja wa Namfua mjini Singida.
Kundi
B, Allicane FC watawakaribisha AFC ya Arusha uwanja wa CCM Kirumba, JKT
Rwamkoma watacheza dhidi ya Madini FC uwanja wa Karume Musoma, Kundi C,
Changanyikeni dhidi ya Karikoo ya Lindi watacheza katika uwanja wa Karume
jijini Dar es salaam.
Mechi
hizo zitaendelea kwa Kundi D, ambapo African Wanderes watawakaribisha Sabasaba
FC uwanja wa Wambi, Mafinga, Mkamba Rangers dhidi ya Mbeya Warriors uwanja wa
CCM Mkamba, na Wenda FC watacheza dhidi ya Mighty Elephant uwanja wa Sokoine
jijini Mbeya.
Ligi
hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa michezo mitatu kuchezwa katika kundi B, na
C, Pamba FC watawakaribisha Bulyanhulu FC uwanja wa CCM Kirumba, Mshikamo dhidi
ya Abajalo uwanja wa Mabatini, Mlandizi na Villa Squad kuchuana dhidi ya
Comsopolitan uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Chapisha Maoni