Ghana na Ureno nje Brazil2014
Cristiano Ronaldo aliifungia
ureno bao la ushindi timu yake ilipoilaza Black Stars ya Ghana 2-1
katika mechi ya mwisho ya makundi.
ishu ni kuwa Ureno ilikuwa keshabanduliwa nje ya kipute hicho baada ya kushindwa mechi zao za kwanza.Ghana itajilaumu yenyewe kwa kushindwa kusajili ushindi uliohitajika kuihakikishia nafasi katika 16 bora baada ya John Boye alipojifunga mwenyewe.
Asamoah Gyan alifunga bao la kuisawazishia Black stars lakini haikutosha kuifufua kampeini yao kwani walihitaji ushindi wa aina yeyote na kuomba kuwa Ujerumani ishinde marekani iliwaweze kufuzu kama washindi wa pili katika kundi G.
Ronaldo hata hivyo atamshukuru kipa wa Ghana Fatawu Dauda kwa sifa alizopata baada ya kufunga bao la ushindi kufuatia kipa huyo kumzawadia mpira katika eneo la lango naye akaifuma kimiani.
Marekani walijiunga na ujerumani katika mkondo wa pili licha ya Ujerumani kuibana marekani kwa bao moja bila ya jibu.
Ghana hata hivyo ilikuwa tayari inakumbwa na kashfa ambayo wachezaji wake wa kutegemewa Kevin Prince Boateng na Sulle Muntari walitimuliwa kambini huku wale waliosalia wakitishia kususia mechi hiyo ya Ureno kufuatia ubishi kuhusiana na malimbikizi ya marupurupu yao.
kwa upande mwingine
Algeria imefuzu kwa raundi ya pili ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza katika historia ikiwa ni timu ya pili toka Afrika kwa mwaka huu wa 2014.
Algeria itaingia katika kumbukumbu za historia ya Soka Afrika kuwa mwakilishi wa 6 kuwahi kufuzu kwa raundi hiyo ya 16 bora nyuma ya Cameroon Ghana Nigeria Morocco na Senegal .
Hata hivyo vijana wa kocha Fabio Capello walianza kulinda ngome yao mapema bila ya tahadhari kuwa baop lolote la Algeria ingewarejesha nyumbani.
Mashambulizi ya Algeria yalizaa matunda kunako dakika ya 60 Islam Slimani alipoisawazishia Algeria kutokana na mkwaju wa freekick uliopigwa na Yacine Brahimi.
Wadau watachunguza tukio ambalo shabiki mmoja anadaiwa kumulika kifaa cha Laser usoni mwa kipa wa Urusi Igor Akinfeev kabla ya bao hilo la kusawazisha.
Urusi ilifanya mashambulizi kwenye lango la Algeria lakini wapi safu ya ulinzi ilikaa ngangari na kuhimili mashambulizi hadi kipenga cha mwisho na hivyo kuipa Algeria alama moja muhimu iliyoiwezesha kuweka historia ya kufuzu kwa raundi ya pili ya kombe la dunia.
Algeria sasa imeratibiwa kukwaruzana na Ujerumani katika mechi ya 16 bora siku ya jumatatu.
BY BBC NETWORK.
Chapisha Maoni