Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.






TIMU ya Lipuli imeadhimia kutanua  matawi ya timu hiyo ili kuhakikisha timu hiyo inakuwa na wanachama wengi kama ilivyo kwa simba na Yanga mpango ambao utapelekea timu hiyo kujiimalisha kimapato na kuwa na uwezo wa kujiendesha yenyewe.

Akizungumza na jelamba viwanja naibu katibu wa Lipuli Ronjino Milambo alisema kwa kuanzia kila eneo lenye wanachama zaidi ya ishirini watakuwa na tawi lao hali ambayo itapelekea wanairinga wengi kujiunga katika matawi mbali mbali ya timu ya Lipuli kulingana na maeneo wanayoishi.

“Hadi kufikia hivi sasa timu yetu inawanachama zaidi ya 70 lakini wanachama waliolipia kadi zao ni chini ya 35,ambapo kama matawi ya lipuli yataongezea tukakuwa na wanachama wengi zaidi”alisema milambo

Hivi karibuni Lipuli imepitsha Rasmu ya kuundwa kwa kamati ya Maadili ambayo itasaidia timu hiyo kuendeshwa kisasa kwa kufuata taaluma ya soka.


Chapisha Maoni