Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Mapinduzi cup kutimua vumbi mwenzi wa nane.

Michuano ya mapinduzi cup Wilayani mfindi inatarajia kutimua vumbi mwenzi wa nane mjini mafinga ambapo maandalizi ya michuano hiyo yanaendelea vizuri na jumla ya timu 25 zitajitupa uwanjani wilayani humo.
Akizungumza na Championi Ijumaa mratibu wa mashindano hayo Mapinduzi Shabani alisema kuwa lengo kuwa la kuandaa michuano hiyo kila mwaka ni kuamasisha jamii kupanda miti,chai pamoja na kutunza mazigira ya wilaya hiyo kwa kuwa michezo inakutanisha watu wengi kwa wakati mmoja.
“licha ya kuibua vipaji vya mpira vile vile tuna lengo la kutoa elimu kwa jamii kuhusu kutuza mazingira pamoja na kufanya shughuli za kimaendelea ambapo tunawahasa wanamfindi wote kuhudhulia kwa wingi katika mashindano hayo.
Katika kinyang’anyiro hichio mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha shiringi milioni mbili kasha wa pili milioni moja na watatu atachukua laki Tano.
Wakati huo huo

TIMU ya soka ya Mkali Kids Wilayani nyasa ipo katika maandalizi ya mwisho ya kujiandaa na ligi Daraja la nne wilayani humo michuano ambayo inatarajia kuanza tarehe 26 mwenzi huu ambapo timu hiyo imepania kuwa bingwa na kupa nafsi ya kusonga mbele katika mashindano hayo.
Kocha mpya wa timu hiyo muddy Songambele ambaye zamani alikuwa kocha wa nyasa Fc alisema kikosi chake kina wachezaji wazuri na lengo kubwa ni kuifikisha timu hiyo katika ligi ngazi ya mkoa na kuendelea ili kuhakikisha wilaya ya nyasa inapata nafsi ya kushiriki mashindano makuwa licha ya kuwa mara nyingi timu za wilaya hiyo zinaishia ngazi ya mkoa.

“licha ya kukabidhiwa timu hii hivi karibuni lakini naamini tutafanya vizuri kwa kuwa mpira ni kujituma na kuwa na wachezaji wazuri vitu ambavyo kikosi changu  kimebarikiwa kuwa navyo,pia wilaya ya nyasa imebarikiwa kuwa na wachezaji wenye vipaji lakini mara nyingi wanaishia ukingoni kwa tatizo la udhamini ambapo wadau wasoka na wapenda mpira lazima watupie jicho ziwani humo.


Chapisha Maoni