Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Kandanda ni miongoni mwa michezo maarufu duniani kutoka nan a mchezo huu kuwa na wadau na mashabiki wengi ambao wanafuatilia mchezo huu kila pembe duniani kote,licha ya kuwa na umarufu mkubwa mchezo huu mara nyingi umekuwa ukiusishwa na matukio mengi ya kishirikina.

Hebu leo hii tujikumbushe matukio machache yaliyowai tokea hapa nchini katika viwanja mbali mbali ambayo yaliambatana na imani za kishirikina.
Mwaka 1983 kulikuwepo na mechi kali sana kati ya maji maji na Simba toka jijini Dar es salam mechi hile ilichezwa wakati kamati ya ufundi ya Simba ilikuwa inaongozwa na kikosi ambacho kilikuwa imesheni vichwa toka Brazil na wakati huo Simba ilikuwa imezindua mfumo mpya wa kibrazili maarufu Kama ‘Kanivo Samba’ hakika simba ile ilikuwa ikitisha hapa nchini.

Kipindi hicho maji maji ilikuwa na mlinda mlango maili toka hapa Iringa wengi tunamfahamu anaitwa ISIHAKA MAJALIWA ambaye alikuwa tegemeo kwa wanalizombe kipindi hicho maji maji ilikuwa tishi kwa vigogo simba na yanga hapa nchini,basi siku moja kabla ya mechi viongozi wa maji maji walimuchukua majaliwa na kupeleka kwa mganga kwa lengo kufanyiwa dawa ili kuwazuia simba wasipate ushindi katika mchezo huo ambapo mganga huyo kwa sasa ni marehemu.

Uwezi kuamini! asubuhi siku ya mchezo mganga alimwambia majaliwa kuwa mchezo wa leo utakuwa mgumu sana lakini nimejitaidi sana leo usiku kuokoa magoli ambayo yalikuwa yakiingia langoni kwetu hata hivyo yamebakia mawili hayo nitamalizia uwanjani wakati mechi ikiendelea.

Kipa wa Maji maji isihaka majaliwa alipuuzia maneno yale kwa kuwa yeye alikuwa akimtegemea mungu,kipindi chote ambacho alikuwa akicheza mpira pia alikuwa akiwaeshimu simba kwa mchezo mzuri ambao walikuwa wkicheza, ama hakika simba walikuwa tishio.

Mchezo ulianza kwa kasi huku simba wakiwashambulia vilivyo wenyeji wao maji maji ya songea ambapo simba walipata bao la kwanza mwamzi akakataa,wakatapata bao linguine mwamzi akakata tena akidai kuwa wachezaji wa simba waliotea ambapo hadi mwisho wa mchezo licha ya simba kufunga bao mbili za wazi  maji maji 0-simba mtungi hapo ndipo majaliwa ilipokumbuka maneno yam ganga na akahamini kuwa katika mpira uchawi upo.
Uchawi noma lakini ngoja tugeukie kwa wazee wa jangwani yanga mwaka 1988 katika mchezo ambao walikwaaana na coastal unioni ya Tanga  mechi ambayo ilifanyika kwenye uwanja wa taifa jijini dar es salam maarufu kama shamba la bibi.
Anasimulia mwana makata kocha wa JKT oljolo ya sasa

“Nakumbuka mwaka 1988 nikiwa na Yanga siku chache kabla ya  mchezo wetu wa mwisho na Costal Union ya Tanga walikuja waganga wapatao 10,Toka mikoa Tofauti kwa ajiri ya kutufanyia dawa ili kupata ushindi katika mechi yetu na wachezaji wote tulilazimishwa kushiriki tukio lile kuanzia saa 3 usiku hadi saa 8 usiku lakini licha ya kutumia dawa zile Tulikung’utwa bao 1-0,na Wagosi wa kaya wakatangazwa kuwa mabingwa wa Tanzania kwa mara ya kwanza na sisi tukamabulia nafasi ya pili.


Kikosi cha yanga ambacho kilikosa ubingwa mara baada ya kukesha kusiku kucha na wataalamu wa mitisha toka kwa wataalam wa miti shamba ni kama ifuatavyo
Golini alikuwepo mwana makata
,2 Lawrenc MwaluSako,
3 Fred Felix,
4 Godwin Aswile,
5 Said mwamba6,
6 Issa Athuman,
7 Abuu Bakari,
8 Athuman China,
9 Abeid Mziba,
10 Edga Fungo na
11 ni Celestin Sikinde
Kweli mpira mazoezi na ujuzi wa mwalimu na sio kamati ya ufundi nje ya uwanja.  


Chapisha Maoni