Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Chuo kikuu kishiriki cha mkwawa mkoani Iringa kinatarajia kuandaa mashindano ya michezo mbali mbali ya kumwezi mtwa mkwawa yatakayofanyika tarehe 24 mwenzi wa kumi na moja  mwaka huu.

Michezo ambayo itakuwepo katika mashindano hayo ni pamoja na mpira wa miguu,riadha,mpira wa pete,kikapu na michezo mengine mengi baada ya kupata udhamini katika mashindano hayo.

Akizungumza na Jelamba viwanjani hii leo waziri wa michezo serikali ya wanafunzi mkwawa  maguluko dogulas alisema kuwa wanakaribisha makampuni mbali mbali mbali kudhamini mashindano hayo ili kuweza kufanikisha mashindano hayo kwa asilimia zote kwa kuwa bila udhamini watashindwa kufikia malengo ya mashindano hayo.

Kwa upande wake Anna Thalia mwalimu wa chuo kikuu cha mkwawa aliongeza kuwa chuo cha mkwawa toka kianzishwe wamesoma wanafuzi wengi sana ambapo kuanzishwa kwa mashindano hayo itapelekea kuwepo kwa umoja na mshikamano pia kuhamasisha wanadu toka maeneo tofauti kuwachangia wanafunzi ambao wanasoma katika mazingira magumu chuoni hapo   ili kuwawezesha kumalizi vizuri masomo yao.

Michuano hiyo itajumuisha timu mbali mbali za vyuo vyote toka mkoani Iringa.



Chapisha Maoni