Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Maji maji waanika kikosi chao






Na Alex Mapunda,Iringa
TIMU ya soka ya Maji Maji toka Mkoani Ruvuma tayari imeshakamilisha  usajili wa wachezaji 26 na wanatarajia kuingia kambini muda wowote kuanzia hivi sasa ili kujiwinda na ligi daraja la kwanza.

Meneja wa timu hiyo God Mvula amesema ili kujiandaa vema na michuano hiyo timu ya Maji Maji itashiriki michuano ya Super Cup ambayo imeandaliwa mjini Songea,mashindano ambayo yanashirikisha timu za ligi ya  daraja la tatu na daraja la kwanza wakiwemo Mlale Jkt toka Songea vijijini ambao nao wanashiriki ligi daraja la kwanza.


Mvula amekitaja  kikosi cha wachezaji 12  wapya wa maji maji ambao ni Oswald Issa, Samir Said, Emmanuel Maganga, Ally Mohamed, Kudra Omary, Said Fundikira, Mrisho Said, Idd Kipagule, Mohamed Omary, Yohana Kimburu na Msafiri Abdallah.



 wachezaji wa zamani 14 watakaoendelea kuitumikia klabu hiyo kuwa ni pamoja na Anthony Mwingira, Eliuta Ndunguru, Bahati Yussuf, Gerarrd Mbena, Abdallah Aus, Ditram Nchimbi, Filoteus Mahundi, Mpoki Mwakinyuke, Alex Zegega, Sadiq Gawaza, Odo Nombo, Frank Sekule, Marcel Boniventure na Freddy Mbuna.

Kindumbwe ndumbwe cha ligi daraja la kwanza kinatarajia kutimua vumbi tarehe 14 mwenzi wa kumi ambapo safari hii kutakuwepo na makundi mawili na Kundi A lina timu za African Lyon, African Sports, Ashanti United, Friends Rangers, Kimondo SC, Kurugenzi Mafinga, Lipuli, Majimaji, Mlale JKT, Polisi Dar es Salaam, Tessema FC na Villa Squad.

Wakati kundi B lina timu za Burkina Faso, Geita Veterans SC, Green Warriors, Kanembwa JKT, Mwadui SC, Oljoro JKT, Panone FC, Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Tabora, Rhino Rangers na Toto Africans. Ratiba ya Ligi hiyo itatolewa hivi punde.


Chapisha Maoni