TIMU ya soka ya lipuli ya Iringa
Imeanza vibaya michuano ya ligi daraja la kwanza baada ya kutandikwa bao 2-1
dhidi ya Friends Rangers ya Manzese Toka Dar es salam katika mchezo ambao ulifanyika hivi karibuni
kwenye uwanja wa Karume jijini humo.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa
kusisimua Lipuli ilikuwa ya kwanza
kupata bao dakika ya 30 kupitia kwa Abdallah Mussa, kabla ya Yussuf Mkinda
kuiswazishia Rangers dakika ya 34 kwa penalti kufuatia mchezaji wa Lipuli,
kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Rangers ilipata bao lake la ushindi kupitia kwa mshambuliaji wa zamani wa Simba SC na Mtibwa Sugar, Yusuph Mgwao , dakika za lala salama ambapo hadi dakika 90 za mchezo lipuli wakatoka uwanjani vichwa chini baada ya kukosa pointi tatu muhimu.
Baada ya mchezo huo mwenyekiti wa timu
ya soka ya Lipuli Renatus Karinga, ambayo ilifanya vizuri miaka ya
1990,alilalamikia bao la pili la mchezo huo akidai kuwa mwamuzi aliwabeba
wapizani wao kwa kuwapa penalti hiyo.
“Tumeonewa,penalti haikuwa ya
kweli,waamuzi bado ni tatizo kwa soka letu hapa nchini hasa kwenye ligi za
madaraja ya chini timu zikiwa ugenini zinaonewa sana” alisema karinga.
nayo kurugenzi ya mafinga imeanza kwa ushindi baada ya kuifumua Sessema fc bao 2-0
Chapisha Maoni