Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Muogeleaji bingwa wa Olimpiki nchini Marekani,Michael Phelps, amekamatwa kwa kundesha gari akiwa mlevi.
Polisi mjini Baltimore, katika jimbo la Maryland, wamesema kuwa Phelps alisimamishwa kwa kuendesha gari kwa kasi kupindukia Jumanne asubuhi akiwa mlevi.
Bwana Phelps hakukataa kushirikiana na polisi aliposimamishwa na kuchunguzwa ikiwa alikuwa timamu. Alishitakiwa na kuachiliwa.
Muogeleaji huyo anayesifika sana aliwaomba radhi mashabiki wake kupitiaTwitter.
"naelewa ukubwa wa kosa langu na ninawajibika sana,'' aliandika Phelps.
''Najua maneno haya huenda hayamaanishi chochote kwa sasa lakini ninawaomba radhi kwa yeyote ambaye nimemuangusha.''
Bwana Phelps, mwenye umri wa miaka 28, alijiuzulu kutoka kwa mashindano ya uogeleaji, baada ya kushinda medali yake ya 22 kwenye mashindano ya olimpiki, katika mashindano yaliyofanyika mjini London mapema mwaka huu.
Polisi walimkamata Phelps na kumshitaki kwa kosa la kuendesha gari kwa kasi akiwa mlevi.
Taarifa ya polisi ilisema kuwa Phelps alishirikiana na polisi kutoka mwanzo hadi mwisho alipoachiliwa baada ya kushtakiwa.
Phelps ashawahi kushitakiwa kwa kosa lengine sawa na hilo mwaka 2004. Alikiri kosa na kuepuka kifungo cha nje ya miezi 18.
by bbc


Chapisha Maoni