kenyaTimu ya Gor Mahia nchini Kenya
ndio mabingwa wa Ligi msimu huu baada ya kuishinda kilabu ya Ushuru mabao 3-0.
Wakicheza mechi yao ya mwisho ya
msimu huu Gor kwa jina maarufu K'Ogalo walihitaji kuishinda KRA ili kushinda
taji hilo katika mechi hiyo iliyochezewa katika Uwanja wa Moi mjini Kisumu.
Licha ya timu zote mbili kuonyesha
mchezo mzuri hususan KRA, mkwaju wa Eric Ochieng mwisho wa dakika za lala
salama katika kipindi cha kwanza, na bao lililofungwa dakika chache za kipindi
cha pili na mashambuliaji Dan Sserenkuma bila kusahau bao la tatu la Simon
Mburu yalifanya mambo kuwa 3-0.
Katika uwanja wa Ruaraka jijini
Nairobi,Elly Kalekwa na kikosi chake cha Sofa Paka walidhani kwamba
wataicharaza Tusker FC huku nayo Gor Ikishindwa na wana Ushuru ili kuweza
kubeba kombe hilo.
Lakini mambo yalienda segemnege
upande wa batoto ba Mungu kama wanavyojiita Sofapaka ambao walipata sare ya 2-2
dhidi ya Tusker na hivyobasi kuyafanya mambo kuwa magumu zaidi.
NO | Team | M | PT |
1 | Gor Mahia | 30 | 60 |
2 | Sofapaka | 30 | 57 |
3 | Tusker FC | 30 | 53 |
4 | Ulinzi Stars | 30 | 51 |
5 | Chemelil Sugar | 30 | 48 |
6 | AFC Leopards | 29 | 41 |
7 | Muhoroni Youth fc | 30 | 40 |
8 | Thika United | 30 | 39 |
9 | SoNy Sugar | 29 | 38 |
10 | Mathare United | 30 | 38 |
11 | Western Stima | 30 | 36 |
12 | Ushuru FC | 30 | 33 |
13 | Bandari | 30 | 30 |
14 | KCB | 30 | 29 |
15 | Nairobi City Stars | 30 | 24 |
16 | Top Fry AllStars | 30 | 17 |
Chapisha Maoni