Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 
NA Alex Mapunda,Iringa
MICHUANO  ya ligi daraja la kwanza ikiwa inaendelea kushika kasi,hivi karibuni timu za mkoa wa Iringa zimevutwa mashati mara baada ya kulazimishwa sare katika mechi zao.

Katika mchezo ambapo ulipigwa katika uwanja wa Wambi Mafinga timu ya kurugenzi ilitoka sare ya  bao 1-1 na friends Rangers kutoka  Jijiji Dar es salam katika mchezo ambao ulikuwa mgumu na kuvutia,huku Lipuli ya Iringa ikitoka Sare ya bila kufungana mchezo ambapo ulifanyika katika uwanja wa karume Jijini Dar es salam.

Akizungumzia mchezo  huo  katibu Msaidizi wa Lipuli Ronjino Malambo amesema  kikosi chao kimezidi kuonyesha ukomavu wa hali ya juu ambapo kwa sasa wanajipanga  kukabiriana na Tessema Fc pamoja na Kurugenzi michezo ambayo itachezwa mkoani Iringa.

Kwa upande wake katibu mkuu wa kurugenzi amesema bado timu yao inanafasi kubwa ya kufanya vizuri katika ligi hiyo kwa kuwa wao wanashika nafsi ya nne kwa kufikisha pointi 12 ambapo anaeongoza ligi Maji Maji ya Songea anapointi 16.


Chapisha Maoni