Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 IRINGA

Na Alex Mapunda,Iringa
BAADA ya kuendeleza wimbi la sare  wadau na wapenzi wa Kandanda mkoani Iringa wameanza kujiuliza maswari ili kubaini palipo na mapungufu ili kuongeza nguvu na kujipanga vema mzunguko wa pili.
Akizungumza na chanzo kocha aliyeng’ara na Lipuli Miaka ya nyuma Pascal Bella amesema kwa sasa lipuli inatakiwa kuangalia mapungufu yaliyopo na kuyaziba kwa kufanya usajili mzuri ili kuimalisha kikosi hicho mzunguko wa pili.
“Hali ya timu ni zuri ila ushauri wangu ni kwamba wakati wa mapumziko kuelekea mzunguko wa pili kambi ya timu hiyo isivunjwe ili kuendelea kukijenga kikosi hicho pia uongozi ukae na wadau wa mpira,kwa kuangalia mapungufu yaliyopo  ili kujipanga vyema na mzunguko wa pili kwa kuwa nafsi ya Lipuli kucheza ligi kuu bado hiyo”.
Bella aliongeza kuwa wadau na wapenzi wa timu hiyo waendelee kuwa pamoja na timu  ili kuhakikisha  wanaiunga mkono timu yao kwa asilimia zote kwa kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu .
Katika msimamo wa ligi kundi A Lipuli wamefikisha pointi Kumi 14 na wamebakisha mchezo mmoja dhidi ya kurugenzi mchezo ambao utakamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi  daraja la kwanza kwa upande wao.


Chapisha Maoni