Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 
Na Alex Mapunda,Iringa
TIMU ya Maji Maji toka Mkoani Ruvuma imeendelea kung’anga’nia  kileleni mwa ligi daraja la kwanza kundi A baada ya hivi karibuni kupata ushindi mnono dhidi ya watani wao wa jadi Jkt Mlale Toka songea vijijini wa bao 2-0 Katika mtanange wa ligi daraja la kwanza uliofanyika kwenye uwanja wa Maji Maji songea.
Mchezo huo ambao ulikuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na uhasama uliopo baina ya timu hizo Maji Maji iliwachukua dakika 25 pekee kabla ya Mrisho Said kupachika bao  la kwanza ambao lilidumu hadi kipindi cha kwanza kilipomalizika.
Kipindi cha pili Maji Maji waliendelea kuwasha moto  kwa kucheza kandanda safi la kuvutia na mnamo Dakika ya 75 kipindi cha pili mchezaji maili Alex Kondo alifunga bao Safi mara baada ya kupokea pasi safi toka kwa Mkongwe Fred Mbuna ambapo hadi dakika 90 zilipokatika wanalizombe wakaibuka na ushindi wa bao 2-0.
Akizungumza na championi Jumatatu Meneja wa Maji Maji God Mvula alisema baada ya mchezo huo Mshabika wa timu ya maji maji waliungana kwa pamoja huku wakiimba Maji Maji ligi kuu na hakuna wa kuwasimamisha.
Maji Maji katika kunda A wanaongoza kwa kufikisha pondi 21 na wamebakiza Mchezo mmoja mzunguko wa kwanza dhidi ya Kimondo Toka mbozi mbeya ambapo katika kundi hilo wananyemelewa na Friend Rangers wenye pointi 19.


Chapisha Maoni