Upangaji wa makundi ya timu kumi na
sita zilizofuzu kucheza fainali za mashindano ya 30 ya kuwania Kombe la Mataifa
ya Afrika kwa mwaka 2015 yamefanyika katika mji mkuu wa Equatorial Guinea,
Malabo.
Mashindano hayo yataanza Januari 17,
2015.
Upangaji wa makundi ulirudishwa wiki
moja nyuma ili kuiwezesha Equatorial Guinea, kujiandaa baada ya kuchukua nafasi
ya Morocco, iliyokuwa iandae mashindano hayo, lakini ilishindwa kufanya hivyo
baada ya kutaka mashindano hayo yasogezwe mbele kuhofia ugonjwa wa Ebola ambao
umeyakumba baadhi ya mataifa ya Afrika Magharibi, ambako zinatoka timu nyingi
zinazoshiriki michuano hiyo.
Mabingwa watetezi Nigeria ni moja ya
timu kubwa zilizoshindwa kufuzu kucheza fainali za mwakani, pamoja na Misri na
Angola ambazo zote kwa mshangao hazitaweza kushiriki.
Haya hapa makundi manne ya AFCON
2015:
Kundi A Equatorial Guinea, Burkina Faso, Gabon, Congo
Kundi B Zambia, Tunisia, Cape Verde, DR Congo
Kundi C Ghana, Algeria, South Africa, Senegal
Kundi D Ivory Coast, Mali, Cameroon, Guinea
Wenyeji Equatorial Guinea na Congo
zitacheza mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo. Kundi D ndilo linaloonekana kuwa
gumu zaidi kutokana na timu zilizopangwa kundi hilo.
Chapisha Maoni