Mchezaji wa Argentina Franco Nieto
,mwenye umri wa miaka 33 amefariki baada ya kupigwa kwenye kichwa wakati wa
mechi siku ya jumamosi.
Nieto ,nahodha wa kilabu ya kijimbo
ya Tiro federal alishambuliwa na genge baada ya mechi kati ya wapinzani wao wa
jadi Chacarita Juniors katika mji wa Aimogasta kazkazini magharibi mwa
Argentina.
Mechi hiyo ilisimamishwa kwa dakika
15 kabla ya kukamilika baada ya refa kuwapa kadi nyekundu wachezaji wanane kwa
kupigana.
Mwaka huu watu 15 wamefariki katika
ghasia zilizosababishwa na soka nchini Argentina,Binamu wa Nieto,Pablo Nieto
amesema kuwa watu watatu walimzunguka mchezaji huyo alipokuwa akielekea katika
gari lake na mkewe na mtoto wao wa mwezi mmoja.
Walimpiga kwa ngumi na mateke kabla
ya mmoja ya watu hao kumpiga na jiwe katika kichwa na kumwacha bila fahamu.
Alifanyiwa upasuaji siku ya jumanne
lakini akafariki siku ya jumatano.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo
hilo Fabian Bordon ameviambia vyombo vya habari kwamba watu watatu wamekamatwa
kutokana na shambulizi hilo.
Ghasia zinazosababishwa na soka ni
tatizo kubwa nchini Argentina.
Kulingana na shirika moja lilisokuwa
la kiserikali Salvemos el Futbol,vifo vinavyosababishwa na ghasia za soka
vimeongezeka mwaka huu.
Washukiwa wakuu ni genge la Barras
Bravas ambao hudhibiti maneo ya kukalia katika viwanja vya mpira na barabara
karibu na viwanja hivyo.
http://www.bbc.co.uk
Chapisha Maoni