Shirikisho
la soka FA linachunguza ujumbe wa Instagram wa mshambuliaji wa Liverpool Mario
Balotelli unaodaiwa kuwa ni wa kibaguzi.
Ballotel mwenye umri wa miaka 24
akijibu shutma dhidi yake kutokana na ujumbe wake mtandaoni aliandika tena
ujumbe usemao “mama yangu ni Myahudi wote nyamazeni kimya”.
Hata hivyo Balotelli anadaiwa
kuufuta haraka haraka ujumbe wa awali aliouandika ambao unadaiwa kuwa ni
wakibaguzi.
Msemaji wa Liverpool anayochezea
Balotell amesema kuwa wanataarifa kuhusiana na ujumbe huo na kwamba watafanya
mazungumzo na Balotell.
Shirikisho la soka FA limesema kuwa
linataarifa kuhusiana na mchezaji huyo kuiweka taarifa hiyo katika Instagram na
kisha kuifuta baadae.
Mkurugwenzi wa zamani wa shirikisho
la soka Simon Johnson anasema Balotell anastahili kuchukuliwa adhabu kwa
kitendo hicho
BY http://www.bbc.co.uk
Chapisha Maoni