Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Kiungo mbrazil Emerson De Oliviera Neves Roque (kushoto) akisaini mkataba leo wa kuitumikia klabu ya Young Africans, kulia ni Afisa Habari wa klabu Baraka Kizuguto
Kiungo Emerson De Oliveira Neves Roque jana alisaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia klabu ya Young Africans baada ya benchi la ufundi kuridhika na uwezo wake,na mchezaji mwenyewe kufikia makubaliano hayo ya kuwatumikia watoto wa Jangwani. Baada ya kufanya mazoezi kwa siku nne mfululizo chini ya makocha Marcio Maximo, Leonardo Neiva na makocha wazawa Salavatory Edward, Shadrack Nsajigwa kwa pamoja wameridhiswa na uwezo wake na kuomba apewe kandarasi la kuitumikia klabu ya Young Africans.
Emerson aliyekua akichezea katika timu ya Bonsucesso iliyopo daraja la pili kwenye jimbo la Rio de Janeiro anachukua nafasi ya mshambuliaji Geilson Santos "Jaja" ambaye ameshindwa kureje nchini kutokana na matatizo ya kifamilia na kuomba klabu ya Young Africans imuache.
Kocha wa Young Africans Marcio Maximo amesema wamerizishwa na uwezo na kiungo mkabaji Emerson na kusema ataisaidia timu katika michuano mbali mbali ya Ligi na Kimataifa.
Ujio wa Emerson unafanya klabu ya Young Africans kufikisha jumla ya wachezaji watano wa kimataifa, wengine wakiwa ni Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima, Hamis Kizza na Andrey Coutinho.


Chapisha Maoni