Garry Neville Kushoto na Paul
Scholes kulia
Kocha wa kilabu ya Manchester United
Louis Van Gaal amewaambia wachezaji wa zamani wa kilabu hiyo Gary NevilLe na
mwenzake Paul Scholes kwamba hawajui chochote kinachoendelea katika kilabu
hiyo.
Van Gaal anaiongoza timu yake katika
mechi ya jumapili dhidi ya mabingwa wa zamani wa ligi ya EPL Liverpool huku
Neville akisema kuwa Manchester United inalinda lango lake kama kilabu ya
walevi naye Scholes akisema kuwa anahofia kwamba wachezaji chipukizi katika
eneo la kazkazini mashariki mwa Uingereza huenda wakaelekea katika uwanja mpya
wa kilabu ya Manchester City.
Lakini kocha Van Gaal alimjibu
Neville wiki iliopita akimuonya kujihadhari na matamshi yake.'
'Alisema Neville ,''Jengo na malazi
katika uwanja wa zoezi sio muhimu,kilicho muhimu ni filosofia na wafanyikazi na
baadaye unafaa kutafuta vipaji'',Lakini Van Gaal alimjibu akisema kuwa hana
muda wa kutofautisha wafanyikazi wa Mancity na vipaji ,lakini anapoona kile
walichonacho yeye hufurahi.
Neville alisema baada ya Manchester
United kushinda katika mechi dhidi ya Southampton kwamba mechi ya siku ya
ijumaa itakuwa sawa na kuangalia mbwa na Bata wakicheza dhidi ya simba
mwekundu.
http://www.bbc.co.uk
Chapisha Maoni