Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




IRINGA

Wanachana wa timu ya lipuli ya Iringa hivi karibuni wamekaa kikao na kujadali mambo mbali mbali kuhusu timu yao ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza.

Katika kikao hicho ambacho kiliwakutanisha wanachama pamoja na viongozi wa lipuli wote kwa pamoja warikubariana kuisaidia lipuli kwa hali na mali ili kuhakikisha inapanda daraja msimu.

“timu ipo kambini na wanachama  wamehaidi kuichangia lipuli kwa moyo wote ili iweze kufanya vizuri na kupanda daraja,wakati wa kikao wanachama walichangia laki moja ,pia nawaomba wanairinga wote waendelea kuungana hasa kipesa kwa nmanufaa ya lipuli,alisema katibu msaidi wa Lipuli Ronjino Malambo

Vile vile malambo aliongeza kuwa kutokana na mvutano ambao ulikuwepo katika  uongozi kwa siku za nyuma, wote kwa pamoja wamekubarina kukaa meza moja na kuweka tofauti zao pembeni kwa kuwa kama wanatofautiana kipindi hiki timu inaweza kusambalatika.

Katika msimamo wa ligi daraja la kwanza lipuli inashika nafsi ya tatu ikiwa imefikisha pointi 20 nyuma ya Maji Maji na Friend Rangers ambapo maji maji anaongoza kundi hilo kwa kufikisha pointi 24.



Chapisha Maoni