Ligi
kuu ya England iliendelea tena wikindi hii ambapo kulikuwa na michezo
miwili. Katika mchezo wa awali West Ham United waliwakaribisha Swansea
huku Leicester City wakisafiri hadi Villa Park kuuamana na Aston Villa.
Katika mechi ya awali kati ya West Ham United na Swansea West Ham waliiadhibu Swansea baada ya kumiminia magoli 3 - 1.Magoli mawili ya West Ham yalifungwa na Andy Carrol katika dakika ya 41 na 66 na jingine likafungwa na Diafra Sakho.
Goli pekee la kufutia machozi la Swansea lilitiwa kimiani na Wilfried Bonny.
Mechi nyingine ilikuwa ni kati ya Aston Villa na Leicester City ambapo mechi hii imemalizika kwa Aston Villa kutoka uwanjani kifua mbele baada ya kufunga Leicester City magoli 2 -1
Leicester City ndio waliokuwa wa kwanza kufunga goli lililofungwa na Leonardo Ulloa baada ya mlinda mlango wa Aston Villa kutema mpira.
Chapisha Maoni