Kocha Sylvester
Marsh amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Marsh alikuwa akisumbuliwa na
ugonjwa wa kansa ya koo na hivi karibuni alisafirishwa kutoka Mwanza hadi
jijini Dar es Salaam.
Hata
hivyo, hali ya Marsh aliyewahi kuwa Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Kilimanjaro
Stars pia alizinoa timu kadhaa za Ligi Kuu Bara iliendelea kuwa mbaya kadiri
siku zinavyosonga mbele.
Pamoja na hivyo
suala la afya yake liliendelea kuwa siri kubwa huku baadhi ya wadau wakisumbuka
kutafuta wodi aliyolazwa.
Aliwahi kuugua taabani
na kukawa na taarifa za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumtelekeza. Lakini
baadaye lilikanusha.
Mdau, Abdulfatah
Saleh ambaye ni mmiliki wa Hoteli ya Sapphire Court ya Kariakoo jijini Dar es
Salaam ndiye alijitolea kumhudumia katika matibabu yake.
Ingawa alikuwa
hapendi watu wajue, lakini mdau huyo ndiye alifanya kila, juhudi kuhakikisha
Marsh anapata matibabu bora hadi alipopata nafuu na kurejea kwao Mwanza.
By s jembe
Chapisha Maoni