Timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana wenye umri chini
ya miaka 15 (U-15) imeingia kambini leo katika hoteli ya Itumbi iliyopo
magomeni chini ya kocha mkuu Adolf Rishard kujiandaa na progamu ya vijana
kuwania kufuzu kwa fainali za U-17 mwaka 2017 nchini Madagascar.
Akiongea na waadishi wa habari leo kwenye ukumbi wa
habari wa TFF Karume, mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana Bw. Ayoub Nyenzi
amesema kamati yake imeandaa programu maalumu ya kuwaanda vijana kwa ajili ya
kuichezea timu ya Taifa U-17 mwaka 2017.
TFF imeandaa program hiyo ya vijana U-15 ambao
watakua kambini kwa muda siku 10, wakifanya mazoezi uwanja wa Karume na kucheza
michezo kadhaa ya kirafiki na timu za Azam U17 na shule ya Sekondari Makongo.
Kocha mkuu na timu yake ya U-15 atazunguka mikoa
saba nchini kwa ajili ya kucheza michezo kadhaa ya kirafiki na kungamua vipaji
vingine kwa ajili ya kuboresha timu yake. Mikoa itayotembelewa ni Mbeya,
Mwanza, Morogoro, Arusha, Tanga, na Dar es alaam (Ilala, Kinondoni, Temeke).
Aidha katika kuhakikisha timu hiyo inakua tayari kwa
michuano ya kuwania kufuzu kwa fainali za U-17 mwaka 2017 nchini Madagascar,
timu hiyo ya vijana itafanya ziara ya mafunzo mwezi Disemba mwaka huu katika
nchi za Malawi, Zambia, Zimbambwe, Botswana na Afrika Kusini kwa kucheza
michezo ya kirafiki.
Mwezi Februari 2016 timu hiyo itacheza michezo
miwili ya kirafiki na timu za mikoa ya Dodoma na Mwanza, kabla ya kuelekea
tena katika ziara kwenye nchi za Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya
mwezi Aprili 2016.
Ratiba ya CAF kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika
2017 inatarajiwa kuanza mwezi Juni 2016, ambapo kikosi cha Tanzania kitakua
kimeshapata muda mzuri wa maandalizi kwa lengo la kuhakikisha timu inashiriki
fainali hizo nchini Madagascar 2017.
Fainali za U-17 mwaka 2017 zinatarajiwa kufanyika
nchini Madagascar, huku Tanzania ikitarajia kwa kuwa mwenyeji wa fainali
hizo za vijana U-17 kwa mwaka 2019.
Jumla ya wachezaji 30 wameitwa kuingia kambini,
wachezaji hao ni Kelvin Deogratius, Magazi Dotto, Anthon Shilole (Geita), Sadik
Sud Ramadhani , Mwinchumu Yahya(Tanga),Faraji John, David Mbakazi , Juma Juma,
Pius Raphael, Davison Meddy, Maulid Lembe (Dodoma), Ibrahim Koba (Morogoro).
Wengine ni Abubakar Badru Nassoro, Yusuf B.A.
Khalfani, All Hafidh Mohamed (Kusini Pemba), Joachim Mwenda, Charles Cassiano,
Luqman Shauri (Tanga), Juma Zuberi (Kigoma), Ismail Abdallah (Kusini Pemba),
Robert Philipo (Arusha), Alex Peter, Mohamed Ally, Rashid Kilongola
(Kinondoni), Saad Juma (Mkoa Magharibi), Ibrahim Shamba (Kusini Unguja), Ally
Msengi, Klevin S.Kijili (Mwanza), Frank Abel (Simiyu) na Bryan Jamal.
Chapisha Maoni