Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Meneja wa Manchester United Louis van Gaal anaamini kipa David De Gea atakaa Old Trafford licha ya utata kuhusu mustakabali wake.
De Gea amesalia na mwaka mmoja kwenye mkataba wake Old Trafford na anatarajiwa sana kujiunga na Real Madrid baada ya msimu wa sasa kumalizika.
Mlinda Mlango huyo wa kimataifa wa Uhispania mwenye umri wa miaka 24 tayari amekataa ofa ya mkataba mpya na anaonekana mbioni kurejea jiji lake la kuzaliwa.
Baada ya sare ya 1-1 wiki iliyopita dhidi ya Arsenal, van Gaal alisema hakufikiri anaweza kumshawishi De Gea aendelee kukaa United. 
 
De Gea hatarajiwi kucheza mechi yao ya Jumapili Ligi ya Premia ugenini kwa Hull City wanaokabiliwa na hatari ya kushushwa daraja kutokana na jeraha la misuli ya paja lililomlazimu kuondoka uwanjani mechi dhidi ya Gunners.
Hata hivyo, alipoulizwa iwapo kipa wa zamani wa Barcelona Victor Valdes anaweza kujaza vyema pengo litakaloachwa Mholanzi huyo alidokeza kwamba huenda De Gea asiondoke.
“Ninaamini bado kwamba David De Gea atasalia nasi,” Van Gaal aliambia wanahabari Ijumaa.
“Ninataka kumchezesha dhidi ya Hull City Jumapili kwa sababu ninaamini ni lazima nitumie timu yangu kali zaidi.
“Je, Valdes yuko tayari kuvalia viatu vyake? Nimeshasema tayari kwamba ninaweza tu kusema hilo iwapo David De Gea atakuwa tayari ameondoka. David alishiriki mazoezi leo na tutasubiri kesho tuone hali yake itakuwa vipi.
“Ninafikiri De Gea ni kipa bora. Ni mechi yetu ya mwisho ya msimu. Ninafikiri lazima utumie timu yako hatari zaidi kwa sababu ni muhimu kwa Hull.
“Mwanzo lazima tusubiri tuone iwapo De Gea ataondoka. Kisha tutazungumza kuhusu mambo hayo mengine.”
Van Gaal pia alifichua kwamba atazungumza na wachezaji kadha United wanaokabiliwa na hatari ya kutemwa siku chache zijazo.
Straika wa Uholanzi Robin van Persie, fowadi wa kukopeshwa kutoka Monaco Radamel Falcao na chipukizi Adnan Januzaj na James Wilson wote wanadhaniwa kutokuwa salama Old Trafford.


Chapisha Maoni