Timu ya taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) imewasii salama leo alfajiri ikitokea nchini Afrika Kusini
ilipokua ikishiriki michuano ya Kombe la Cosafa, baada ya kutolewa katika hatu
ya awali ya makundi.
Stars ambayo jana jioni
ilipoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Lesotho baada ya kufungwa bao 1 - 0,
imerejea baadaa ya kupoteza michezo yote mitatu ya kundi B, baada ya kufungwa
na Swaziland, Madagascar na Lesotho.
Huo
ulikuwa mchezo wake wa tatu katika Kundi B ikiwa imepoteza yote mitatu
baada ya kuanza kufungwa na Swaziland 1-0 halafu MAdagascar 2-0.
Mara baada ya mchezo wa jana
dhidi ya Lesotho, kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij alisema amesikitishwa na
matokeo ya timu yake katika hatua hiyo ya awali baada ya kupoteza michezo yote
mitatu.
Nooij alisema, mpira wa miguu
umebadilika kwani matarajio yake yamekua tofauti, kwani kiwango walivyoonyesha
wapinzani wake katika kundi B vimemstajaabisha.
“Mpira wa sasa hautazami nani
yupo juu katika renki za FIFA, tulikua na matarajio ya kufanya vizuri katika
michuano hii lakini baada ya dakika ya 90 za kila mchezo matokeo hayakua mazuri
kwetu,” alisema Nooij.
Kuhusu kufuzu kwa AFCON 2017,
Nooij amesema katika kikosi chake alichokwenda nacho Cosafa alikua na wachezaji
saba aliowapandisha, anaamini wamepata uzoefu, na sasa atawajumuisha na
wachezaji ambao hawakuweza kushiriki michuano hiyo kujiandaa na mchezo dhidi ya
Misri.
Taifa Stars inatarajia kucheza
kucheza mchezo wake wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa AFCON 2017 dhidi ya Misri,
tarehe 14 Juni 2015 katika uwanja wa Borg el Arab jijini Alexandria.
Chapisha Maoni