Kamati ya uchaguzi ya Chama cha Soka mkoa
wa Dar es Salaam (DRFA), imeshindwa kutekeleza agizo la lililotolewa na mwenyekiti
wa kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) la kusimamisha
mchakato wa uchaguzi wa chama cha soka wilaya ya temeke TEFA uliopangwa
kufanyika jumapili agosti 23/2015.
Baada ya kupitia kwa umakini kanuni za
uchaguzi za TFF za mwaka 2013 ibara ya 6, na kujiridhisha kuwa hakuna kipengele
chochote kinachoruhusu kamati ya uchaguzi ya TFF kuingilia kati mchakato wa
uchaguzi wa TEFA, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya DRFA, Rashid
Saadallah, (mwanasheria), amemuandikia barua mwenyekiti wa uchaguzi wa
TFF, Aloyce Komba kumjulisha hilo.
Komba ameelezwa kuwa mchakato huo sasa utaendelea
kama ulivyopangwa kufanyika jumapili agosti 23/2015.
Mwenyekiti huyo wa uchaguzi DRFA, amesema
mpaka sasa taratibu na maandalizi yote kuelekea uchaguzi huo wa Jumapili
yamekamilika ikiwemo usikilizwaji wa rufaa mbalimbali na kuzitolea uamuzi,hivyo
kitendo cha kuingilia kati mchakato huo ni kinyume cha utaratibu,kwa kuwa
TEFA ni mwanachama wa DRFA na siyo wa TFF.
IMETOLEWA NA MSEMAJI WA DRFA, OMARY KATANGA
Chapisha Maoni