Mshambuliaji raia wa Senegal Papa
Niang ameshawasili jijini Dar es Salaam leo taayari kwa ajili ya kuanza
majaribio yake ya kujiunga na klabu ya ‘Wekundu wa Msimbazi’ Simba SC.
Niang leo ataunganishwa moja kwa
moja na kikosi cha Simba ambacho kitafanya mazoezi yake kwenye uwanja wa
Boko ambako ndipo kikosi hicho kinafanya mazoezi yake kwa ajili ya
kujiandaa na mechi za ligi kuu Tanzania bara inayotarajiwa kuanza
Septemba 12 mwaka huu.
Katika majaribio yake, endapo
Niang ataonesha kiwango cha kumvutia kocha mkuu wa Simba Dylan Kerr
pamoja na benchi zima la ufundi la kikosi hicho, basi huenda akapewa
mkataba wa kuitumikia klabu hiyo ambayo imekuwa ikihaha kutafuta
washambuliaji wa kigeni.
Hivi karibuni Simba ilimleta
mshambuliaji wa kigeni kutoka Burundi Kelvin Ndayisenga ambaye alicheza
kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya URA FC ya Uganda huku
akifanikiwa kuifungia timu hiyo goli moja kwenye ushindi wa goli 2-1.
Inasemekana Simba imeachana na
mshambuliaji huyo baada ya kushindwa kufikia makubaliano katika masuala
ya pesa ambapo Ndayisenga alitaka dau kubwa Simba wakashindwa kufikia na
kuamua kumruhusu aondoke.
Dondoo kuhusu Niang
Jina kamili: Papa Niang
Tarehe ya kuzaliwa: 5Disemba, 1988 (miaka 26)
Mahali alipozaliwa: Matam Senegal
Urefu: Mita 1.81
Nafasi anayocheza: Mshambuliaji
Klabu alizowahi kuzitumikia:
Kwasasa: Mchezaji huru
2005-2006: ASC Thies
2007: FC OPA
2008: AC Oulu
2009-2012: FF Jaro
2013: FC Vostok
2013-2014: Al -Shabab SC
2014-2015: FC Mounana
Chapisha Maoni