Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Dirisha la usajili kwa klabu za Ligi Kuu nchini (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) limefungwa jana ambapo klabu tatu tu za VPL zimeshindwa kuwasilisha usajili wao wa wachezaji katika muda uliopangwa.
Klabu za Coastal Union ya Tanga, Stand United ya Shinyanga na Toto African ya jijini Mwanza zimeshindwa kuwasilisha usajili wao wa wachezaji, faini ni laki tano (500,000) kwa kila klabu iliyochelewesha usajili au itakayobadili majina au kuongeza majina baada ya tarehe ya jana.

Awali TFF ilitoa muda wa wiki mbili kwa vilabu vyote nchini kukamilisha usajili, ambapo vilabu 13 vya ligi kuu vimeweza kukamilisha ndani ya wakati, vilabu 24 vya ligi daraja la kwanza, vilabu 24 ligi daraja la pili pia vimeweza kukamilisha usajili wao ndani ya muda uliopangwa.

IMETOLEWA NA BARAKA KIZUGUTO WA TFF


Chapisha Maoni