Sasa ni uhakika kikosi cha Taifa Stars kesho jioni
kinashuka dimbani kuivaa timu ya taifa ya Iaraq.
Stars
itacheza na Iraq katika mechi ya kirafiki ya mazoezi ambayo haina watazamaji.
“Itakuwa
ni mechi ya kirafiki tu, ni mechi mazoezi ili kujiweka fiti. Baada ya hapo
tutarajia kucheza na Libya,” alisema Kocha Mkuu wa Stars, Charles Boniface
Mkwasa.
“Hii ni mechi si kwa ajili ya rank za Fifa au
vinginevyo, ni kw aajili ya kujipima na
kujiweka sawa,” alisema.
Iraq na
Libya nao wamweka kambi katika hoteli kubwa ya The Green Park ambayo Stars
imeweka kambi.
Hoteli
hiyo ipo mlimani kabisa katika mji huu wa Kartepe nchini Uturuki na inamiliki
viwanja vitano vya mazoezi.
Mkuu wa Msafara wa Kikosi cha timu ya taifa, Msafiri
Mgoyi amesema ameridhishwa na kambi ambayo Taifa Stars wameweka.
Mgoyi amesema ameridhika baada ya Stars kuwasili
katika mji mdogo wa Kartepe ambaye uko juu kabisa ya mlima.
Chapisha Maoni