Na Alex
Mapunda,Iringa
UKARABATI wa
uwanja wa Maji Maji Mkoani Ruvuma umeshakamirika na Tayari TFF imetoa mkono wa Baraka
kwa Maji Maji kutumia uwanja huo kwa
mechi za nyumbani.
Akizungumza
na Chanzo cha Gazeti hili toka Songea Meneja wa timu ya Maji Maji God Mvula
alisema uwanja huo umeshakamirika kwa Asilimia mia na siku ya ufunguzi wa ligi
kuu ya Vodacom tarehe 12 watapepetana na
JKT Ruvu toka Pwani katika uwanja wa Maji Maji.
“Uwanja
umekamirika na sisi tumekamirika tupo tayari kwa kazi ili pupeperusha vyema
bendera ya mkoa wetu,kila mechi kwetu ni fainali”alisema Mvula.
Kwa upande
mwingine kocha mpya wa timu ya Maji Maji toka Finland Mike Keeney Holonton anaendelea
vizuri na mazoezi ya timu hiyo na wachezaji wote wanafurahia mafunzo yake.
kwa upande mwingine,TIMU ya
Liuli Stars toka ziwani Nyasa inatarajia kuingia kambini mwishoni wa wiki hii
ili kujiandaa na ligi Daraja la tatu Mkoa.
Licha ya
kuingia Kambini timu hiyo imekumbwa na ukata na inawaomba wadau na wapenzi wa
timu hiyo kwa nchi zima kutuma michango yao ili kusaidia timu.
“Kuna watu
wamehaidi kutuchangia baada ya kupata taarifa zetu kupitia Gazeti la Championi
wiki zilizopita,pia Helman Maklasi ameshatutumia Elfu Hamsini,tunaomba na
wengine waendelee”alisema muddy Songambele kocha wa timu hiyo.
Chapisha Maoni