Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Mmea mmoja unaokula wadudu unatumia nguvu
za matone ya mvua ili kuwakamata wadudu
hao,wanasayansi wamebaini.
Wanasayansi hao kutoka chuo kikuu cha Bristol
wamebaini kwamba matone hayo ya mvua
husababisha mtikisiko katika majani ya mti huo
ambayo yana umbo la mtungi.
Hatua hiyo huwapeleka wadudu katika mfuniko
wa mtungi huo wenye mtego, ambapo wadudu
hao huzamishwa na kuliwa.
Matokeo ya utafiti huo yaliochapishwa katika
jarida la PNAS yanatokana na kamera zenye kasi
na zisizo na mtikisiko mkubwa.
Kwa matumizi ya vifaa hivyo ,daktari Ulrike Bauer
pamoja na wenzake walirekodi kasi na mtikisiko
unayoendelea katika majani ya mti huo baada ya
kuangukiwa na matoni hayo ya maji.
Hatua hiyo ni ya kipekee miongoni mwa mimiea ,
Daktari Bauer anasema.
''Kasi yake ambayo husaidia kuwakamata
wadudu pamoja na vile mmea huo unavyotumia
nguvu za nje ni swala la kushangaza''.



Chapisha Maoni