Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


LIGI KUU VODACOM
MATOKEO:
Jumatano Oktoba 28
Toto African 1 Mgambo Shooting 0
Mwadui FC 2 Yanga 2
Mtibwa Sugar 1 Kagera Sugar 0
Mbeya City 1 Majimaji Fc 1
Ndanda FC 0 Stand United 0
Simba Sc 1 Coastal Union 0

AZAM FC inaweza kupanda kileleni
mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara iwapo itaifunga JKT Ruvu
Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Hiyo inafuatia mabingwa watetezi,
Yanga SC kulazimishwa sare ya 2-2
na Mwadui FC Uwanja wa Kambarage,
Shinyanga jana.
Na Azam FC wenye pointi 19,
wataipiku Yanga SC inayoongoza kwa
pointi 20 ligi hiyo hivi sasa.
Hata hivyo, hilo halitarajiwi kuwa
jambo jepesi, kwani JKT Ruvu
haijashinda mechi hadi sasa msimu
huu na inapambana na kujinusuru na
balaa la kuwafuata ndugu zao, Ruvu
Shooting Daraja la Kwanza.
JKT Ruvu ililazimika kumuondoa
kocha Freddy Felix Minziro na
kumchukua mkongwe, Alhaj Abdallah
Athumani Seif ‘King Kibaden’ baada
ya matokeo mabaya mfululizo.
Na akiwa anaingia katika mchezo
wake wa pili leo tangu aanze kazi,
baada ya kutoa sare na Mtibwa Sugar
wiki iliyopita, King Kibaden
mshambuliaji wa zamani wa kimataifa
wa Tanzania na klabu ya Simba
anatarajiwa kumfurahisha mwajiri
wake, Jeshi la Kujenga Taifa.
Kocha Muingereza wa Azam FC,
Stewart Joh Hall anataka kutumia
vizuri mchezo wa leo kuwaacha Yanga
SC kwa pointi baada ya kwenda nao
‘bega kwa bega’ tangu mwazo wa
msimu.
Lakini tayari kocha huyo wa zamani
wa Sofapaka ya Kenya, amesema
anamuhofia sana mshambuliaji wake
wa zamani Azam FC, Gaudence
Mwaikimba ambaye kwa sasa yuko
JKT.

LIGI KUU VODACOM
Alhamisi Oktoba 2
Prisons v African Sports
JKT Ruvu v Azam FC



Chapisha Maoni