Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Na Alex Mapunda,Iringa

MENEJA wa timu ya Maji Maji God Mvula amesema waamuzi wanaikosesha ushindi timu yao katika viwanja vya ugenini.

Mvula alisema Mechi nyingi walizocheza ugenini waamuzi waliegemea kwa wenyeji ikiwemo mechi dhidi ya Mbeya City.

"Waamuzi wanatunyonga,mechi yetu na Mbeya City sisi tulitangulia kupata bao lakini mwamuzi akatoa penati ya uongozi kwa wapinzani wetu,hali ambayo ilijitokeza pia dhidi ya Mtiwa" Alisema Mvula.

Aidha Mvula amewataka waamuzi kusimamia Sheria za soka katika michezo yote ikiwemo mchezo wao dhidi ya Simba wikendi hii.

Maji Maji inaitaji kujipanga zaidi ili kujihakikishia nafasi ya Kubaki ligi kuu.



Chapisha Maoni