Majina ya viongozi saba watakaowania urais wa shirikisho la kandanda duniani Fifa yametangazwa.
Vigogo hao ni Prince Ali bin al-Hussein, mwenye miaka 39 ambaye ni rais wa shirikisho la kandanda la Jordan.Musa Bility raia wa Liberia mwenye umri wa miaka 48 akiwa ni rais wa wa shirikisho la soka nchi Liberia .
Pia yupo mtendaji mkuu wa zamani wa Fifa, Jerome Champagne, mwenye umri wa miaka 57 ambae ni raia wa Ufaransa.
Katika kinyang'anyiro hicho yupo katibu mkuu wa Uefa Gianni Infantino, raia wa Italia mwenye umri wa miaka 45.
Rais wa shirikisho la kandanda la Asia Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa, ane yupo kwenye mchuano akiwa na umri wa miaka 49.
Mwingine anayewania kiti hicho ni waziri wa zamani wa Afrika Kusini Tokyo Sexwale, mwenye umri wa miaka 62.
Na wa mwisho ni Michel Platini rais wa shirikisho la soka barani ulaya (Uefa) aliyesimamishwa kwa tuhuma za rushwa akipewa nafasi ya kugombea kiti hicho ikiwa adhabu yake ya kufungiwa itaisha kabla ya muda wa uchaguzi.
Jina la mchezaji wa zamani Trinidadi na Tobago, David Nakhid, halikujumlishwa katika orodha hiyo licha ya nyota huyo kusema aliwasilisha jina lake katika kuwania nafasi hiyo.
Uchaguzi mkuu wa Fifa unatarajiwa kufanyika Februari 26 mwakani.
Chapisha Maoni