Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


KEPTENI wa Manchester United Wayne Rooney
ameruhusiwa kufanyiwa Mechi ya Kumuenzi na
mapato yote ya Mechi hiyo kwenda kwenye
Mifuko ya Hisani.
Mechi hii imepitishwa baada ya Mashabiki
kuiomba Klabu kutambua mchango mkubwa
uliotukuka wa Rooney kwa Klabu hiyo.
Sasa Mechi hii itachezwa Old Trafford hao Agosti
3, 2016 dhidi ya Wapinzani ambao watapangwa
baadae.
Akiongelea uamuzi huu, Rooney alisema: “Usiku
wa Mechi utakuwa spesho kwangu na Familia
yangu na nategemea tunaweza pia tukaleta kitu
kimoja au viwili vya kushtukiza!”
Nae Mtendaji Mkuu wa Man United, Ed Woodward
amesema: "Kuanzia Mechi yake ya kwanza
aliyopiga Hetitriki hadi sasa ana Goli 236, Wayne
amekuwa ndio Mtu mkuu
Katika kipindi cha mafanikio makuu ya Klabu!”
Habari hizi zimekuja wakati Oktoba 24 Rooney
alitimiza Umri wa Miaka 30 na katika kipindi
ambacho ananyooshewa kidole kuhusu uchezaji
wake akiwa amefunga Bao 2 tu za Ligi katika
Mechi 9 Msimu huu.
Rooney, ambae alihamia Man United Mwaka 2004
akitoka Everton, ndie Mfungaji Bora wa 3 katika
Man United akiwa nyuma ya Sir Bobby Charlton,
Bao 249, na Denis Law, Bao 237, akiwa 1 tu
mbele ya Rooney.
Mafanikio mengine ya Rooney akiwa na Man
United ni kutwaa Ubingwa wa England mara 5 na
UEFA CHAMPIONZ LIGI mara 1.
Pia amebakisha Mechi 7 tu kuwa Mchezaji wa 10
kwa Man United kufikisha Mechi 500.



Chapisha Maoni