Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Kakaake mkubwa nyota wa timu ya Argentina na
Barcelona Lionel Messi amekamatwa kwa
kumiliki bunduki bila kibali.
Matias Messi alisimamishwa na maafisa wa
polisi wakati wa ukaguzi siku ya jumapili.
Polisi wanasema kuwa Matias mwenye umri wa
miaka 33 alikataa kuonyesha vibali vyake
aliposimamishwa katika mji wa Rosario.
Polisi walilikagua gari lake na kupata bunduki
ambayo Matias ameshindwa kutoa kibali chake
cha umiliki.
Maafisa hao wanasema kulikuwa na mvutano kati
yao na ndugu huyo wa Messi ,ambapo alijeruhiwa
katika jicho huku maafisa hao wakipata majeraha
madogo.
Baadaye alipelekwa katika kituo kimoja cha polisi
mjini Rosario na kuzuiliwa kwa kwa saa nne.
Alikamatwa mara moja kabla ya mwaka 2008
kwa kubeba silaha bila kibali.
Watu wa familia ya Messi pia wanakabiliwa na
madai ya kukwepa kulipa kodi nchini Uhispania.
Lionel Messi na babaake Jorge wote
wanatuhumiwa kuiibia mamlaka zaidi ya yuro
milioni 4 zinazohusishwa na mapato kutokana na
matumizi ya jina lake.



Chapisha Maoni