Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Charles Boniface Mkwasa amepewa mkataba wa
kudumu kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya
Tanzania (Taifa Stars) kwa kipindi cha mwaka
mmoja na nusu kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu
na kumalizika Machi 31, 2017.
TFF Imefikia makubaliano hayo na kocha Mkwasa
baada ya kurudhika na utendaji wake katika
kukinoa kikosi cha timu ya Taifa, ambapo mpaka
sasa ameweza kuingoza Stars katika sare ya
michezo miwili dhidi ya Uganda na Nigeria.
Kufuatia kusaini mkataba huo, Mkwasa atapatiwa
huduma na marupurupu yote aliyokuwa akipewa
kocha aliyeondoka.
Naye kocha Mkwassa ameeleza kufurahishwa na
makubaliano haya na ameahidi kufanya kila
jitihada kuhakikisha kiwango cha Timu ya Taifa
kinapanda.
Aidha Kocha Mkwassa ametoa wito kwa wadau
wa mpira kumpa ushirikiano katika majukumu
yake mapya.



Chapisha Maoni