Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Hatimaye Kocha Charles
Boniface Mkwasa amesaini
mkataba wa mwaka mmoja
kuinoa Taifa Stars.
Mkwasa amesaini mkataba wa
kuinoa Stars ambao utaisha
Machi 31, mwaka huu.
"Kweli nimsaini mkataba,
nawashukuru sana TFF kwa
kuniamini na kunipa jukumu
hili," alisema.
Mkwasa ambaye mkataba wake
na Yanga uliokuwa unaisha
Desemba mwaka huu, amesema
amepanga kuwaanga Yanga
rasmi.
Kocha huyo tayari
ameiongoza Stars kucheza
mechi mbili za mashindano
akiwa kocha wa muda na
aliiwezesha kutoka sare ya
1-1 dhidi ya Uganda katika
michuano ya Chan.
Mechi ya pili, Mkwasa
aliiongoza Taifa Stars
kutoka sare ya bila kufunga
dhidi ya Nigeria katika
mechi ya kuwania kucheza
Afcon.
Sasa kesho atakuwa na
kibarua cha tatu dhidi ya
Malawi kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam
na kitakuwa cha kwanza
kwake akiwa kocha kamili wa
Taifa Stars.
Mkwasa ameichukua Stars
baada ya Mholanzi, Mart
Nooij kushinda na kuifanya
iwe sawa na jahazi
linaloyumba.



Chapisha Maoni