Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Jose Mourinho amedai hataachia ngazi kwa
hiari yake kama Meneja wa Chelsea labda
afukuzwe kazi.
Jana Chelsea, ikiwa Nyumbani kwao
Stamford Bridge, ilitandikwa 3-1 na
Southampton katika Mechi ya Ligi Kuu
England ambayo wao ndio Mabingwa
Watetezi.
Kipigo hicho ni cha 4 kwa Chelsea katika Ligi
katika Mechi 8 ambazo wameshinda 2 tu na
Sare 2 na sasa wako Nafasi ya 16 wakiwa
Pointi 10 nyuma ya Vinara Man City.
Akiongea mara baada ya kipigo cha Jana,
Mourinho alisema: "Nataka niweke wazi.
Kwanza sikimbii. Pili, Kama Klabu inataka
kunifukuza wanifukuze tu ila mimi sitakimbia
wajibu wangu na Timu yangu!"
Mourinho aliongeza: "Kuwa Bingwa kwa
sasa ni ngumu kwa sababu tuko nyuma
mno. Lakini nina hakika tutamaliza tukiwa
ndani ya 4 bora. Msimu ukiwa mbovu
ukimaliza kwenye 4 bora ni sawa."
Mourinho alinena: "Hiki ni kipindi kigumu na
muhimu kwenye historia ya Klabu hii.
Unajua kwa nini? Kwa sababu wakinifukuza
mimi watakuwa wamemfukuza Meneja bora
Klabu hii imewahi kumpata!"
Mourinho ameitumikia Chelsea katika Vipindi
viwili tofauti na cha kwanza ni kile cha 2004
hadi 2007 na kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu
England mara 2.
Kisha Mourinho akarudi tena Chelsea 2013
na Msimu uliopita kutwaa Ubingwa wa Ligi
Kuu England.



Chapisha Maoni