Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Mazembe Imetisha africa, kufuatia mshambuliaji Mbwana Ally
Samata kufunga mabao mawili katika ushindi
wa 3-0 dhidi ya El Merreikh ya Sudan.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania,
amefunga mabao hayo katika mchezo wa
marudiano wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa
Afrika na kuiwezesha TP Mazembe kwenda
fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza
baada ya miaka mitano.
Nyota wa zamani wa Simba SC ya Dar es
Salaam, Samatta alifunga bao la kwanza dakika
ya 53, akimalizia pasi ya Adama Traore kabla
ya kufunga la pili dakika ya 69 kwa pasi ya Yaw
Frimpong.
Mshambuliaji mwingine wa Tanzania, Thomas
Emmanuel Ulimwengu aliyeingia kipindi cha pili
kuchukua nafasi ya Rainford Kalaba alishiriki
bao la tatu lililofungwa na Roger Assale dakika
ya 71.
Mazembe inayosonga mbele kwa ushindi wa
jumla wa 4-2 baada ya awali kufungwa 2-1
Khartoum, sasa itakutana na USM Alger iliyoitoa
El HIlal ya Sudan katika fainali ya Ligi ya
Mabingwa AFrika mwaka huu.
Kikosi cha Mazembe kilikuwa; R. Kidiaba/T.
Ulimwengu dk58, J. Kasusula, Y. Frimpong, J.
Kimwaki, S. Coulibaly, Asante/R. Assale dk46,
B. Diarra, D. Adjei Nii/ M. Bokadi dk85, R.
Kalaba, M. Samatta na A. Traore.
El Merreikh; J. Salim, Ala'a Eldin Yousif, Musaab
Omer, Ayman Saied, Ragei Abdallah, Amir
Kamal, Ramadan Agab, D. Libere/Ahmed Abdalla
dk68, Bakri Al Madina, S. Jabason na F. Coffie/
Omar Bakheet dk69.



Chapisha Maoni