Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


BAADA ya Maji Maji kupokea kipigo kitakatifu toka kwa Simba cha bao 6-1 hivi karibuni, Meneja wa timu hiyo God Mvula amemalizia hasira zake katika mtandao wa Facebook kwa kutupia picha yake inanyoonyesha masikitiko.

Baada ya kutupia picha hiyo baadhi ya mashabiki wa timu wameitaka Maji Maji kujipanga upya wakati wa dirisha dogo, huku wengine wakionyesha kuikataa timu yao.

"Mpira ndio ulivyo,Arsenal alipigwa bao Nane na Manchester United  Sembuse Maji Maji? Tujipange upya wakati wa Dirisha dogo" alisema Sunday Manucho.

Pia Emanuel Mtenga alisema Maji Maji ni timu ya viongozi ambapo wao Kama Mashabiki timu yao haiwezi kufungwa bao 6-1.

Kwa upande mwingine Mwandishi Mkongwe Mkoani Ruvuma Francis Sengo alisema "Football is not Talkingball" akiwa na maana ya mpira unachezwa uwanjani na sio Mdomoni, hivyo viongozi na wachezaji watekeleza majukumu yao kwa vitendo.

God Mvula baada ya kuweka picha hiyo kwenye Mtandao, nae alisema picha hiyo alipigwa na rafiki zake Hotelini pasipo yeye kujua na lengo la yeye kuweka kwenye mtando ni kuonyesha maumivu aliyopata baada ya Maji Maji kufungwa.

"Bao 6 ilibaki kidogo tu kufa kwa presha,nilichokigundua katika mchezo ule wachezaji kutofanyia kazi maagizo ya Mwalimu,pia wengi wao sio wazoefu katika michuano mikubwa" alisema Mvula

Maji Maji haijawai kupata ushindi wa bao mbili,pia katika mechi za ugenini haijawai kuvuna pointi tatu.



Chapisha Maoni