Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


LEO FIFA imetoa Listi ya Ubora Duniani kwa
Mwezi huu na Belgium imeing'oa Argentina na
kuchukua Nambari Wani huku Tanzania ikipanda
Nafasi 1.
Belgium inepanda Nafasi 2 na kushika 1 wakati
Mabingwa wa Dunia Germany wakibaki pale pale
Nafasi ya Pili.
Argentina, waliokuwa Namba 1, wameporomoka
hadi Nafasi ya 3.
Kwa Afrika, Nchi ya juu kabisa kwenye Listi hiyo
ni Ivory Coast ambayo imekaa Nafasi ya 22
baada kushuka Nafasi 1.
Algeria, ambao ndio waliokuwa juu kwa Afrika,
wameshuka nafasi 7 na sasa ni wa 26 na
Jumapili wanaivaa Tanzania kwenye Kombe la
Dunia 2018 huku Tanzania ikipanda nafasi 1
kwenye Listi hiyo ya Ubora na kushika Namba
135.
Listi nyingine ya Ubora Duniani
itatolewavDesemba 3.
10 BORA:
1 Belgium
2 Germany
3 Argentina
4 Portugal
5 Chile
6 Spain
7 Colombia
8 Brazil
9 England
10 Austria



Chapisha Maoni