Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania,
Taifa Stars Jumapili itacheza mchezo
wa kirafiki na timu ya University of
Pretoria (Tucks FC) mjini
Johannesburg, Afrika Kusini ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya mchezo
dhidi ya Algeria Novemba 14, mwaka
huu jijini Dar es salaam.
Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya
progamu ya kocha mkuu, Charles
Mkwasa baada ya kufanya mazoezi
na vijana wake kwa takribani siku nne
mpaka sasa, anahitaji kuona
maendeleo ya kikosi chake kabla ya
kurejea nyumbani kwa mchezo dhidi
ya Mbweha wa Jangwani Algeria.
Stars iliyowasili jijini Johannesburg
jumatatu mchana, imefikia katika
hoteli ya Holiday Inn Express iliopo
katika eneo la Woodmead ambapo
imekua ikifanya mazoezi yake asubuhi
na jioni katika viwanja vya St. Peters
College na kituo cha cha michezo cha
Edenvale.
Kuhusu hali ya kambi, kocha mkuu wa
Stars Charles Mkwasa amesema
anashukru maendeleo ni mazuri vijana
wake wote wapo katika hali nzuri
hakuna majeruhi na wanaendelea na
maaandalizi ya mchezo dhidi ya
Algeria utakaopigwa Novemba 14 jijini
Dar es salaam.
"Dhumuni la kuweka kambi huku ni
kupata nafasi ya kuwaanda vijana
kwa mazoezi katika mazingira mazuri
ikiwamo viwanja vya mazoezi, chakula
na malazi kinachopelekea kuongezeka
kwa umakini katika mazoezi" Alisema
Mkwasa.
"Tumeanza na mazoezi ya kujenga
utimamu wa mwili kwa wachezaji,
nguvu na stamina, pumzi ili
kuhakikisha vijana wote wanakua
katika kiwango sawa (fitness level)
kisha tutaendelea na mazoezi ya
kiufundi kwa siku zilizosalia kabla ya
kurejea nyumbani" aliongeza Mkwasa.
Wachezaji 26 waliopo kambini ni
magolikipa Ally Mustafa, Aishi Manula
na Said Mohamed, walinzi ni Shomari
Kapombe, Juma Abdul, Ramadhan
Kessy, Mohamed Hussein, Mwinyi Haji,
Hassan Isihaka, Salim Mbonde, Kelvin
Yondani na nahodha Nadir Haroub
“Cannavaro”.
Wengine ni Himid Mao, Frank Domayo,
Mudahir Yayha, Salum Abubakar, Said
Ndemla, Jonas Mkude, Salum Telela,
Farid Musa, Saimon Msuva, Malimi
Busungu, Elias Maguri, John Bocco na
Mrisho Ngasa.
Aidha wachezaji Mbwana Samatta na
Thomas Ulimwengu wanaochezea
klabu ya TP Mazembe ya Congo DR,
wanatarajiwa kuungana na kikosi cha
Stars baada ya mchezo wao wa
fainali Ligi ya Mabingwa Afrika
Jumapili dhidi ya USM Alger.



Chapisha Maoni