LIPULI,KURUGENZI ACHENI MIGOGORO
Na Alex Mapunda,
TAREHE,04-04-2014
UONGOZI wa chama cha mpira wa Miguu mkoani Iringa umewataka Lipuli
Pamoja na Kurugenzi kuepuka Migogoro isiyokuwa ya Lazima ambayo
inaatarisha maendeleo ya timu hizo ambazo zinauwania kupanda ligi kuu.
Akizungumza na JELAMBA VIWANJANI katibu wa chama hicho Eliudi Mvela
alisema jambo pekee la kuepuka migogoro ni viongozi wa timu hizo
kuendesha timu hizo kwa uwazi na ukweli ili kueputa malalamiko toka
kwa wadau wa soka ambao ni jukumu lao kuoji pale timu inapofanya
vibaya.
''Kurungezi walifanya vizuri roundi ya kwanza lakini migogoro
imewarudisha nyuma na raundi ya pili wamefanya vibaya, kwa upande wa
lipuli uongozi unalalamikiwa sana na wanachama wa timu kutokana na
kutokuwepo kwa uwazi katika kuongoza timu hiyo, kikubwa kila mtu
akumbuke mjukumu yake.
Mvela akiongeza kuwa wao kama mkoa watahakikisha mshikamano unakuwepo
katika timu hizo pamoja na kuhakikisha timu zinafanya usajili kwa
wakati pia kutafuta wadhamini wa kudumu ili kuhakikisha timu mojawapo
inapanda daraja msimu ujao.
Chapisha Maoni