Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Na Sophia Mwaipyana,Mbeya .

Timu ya Wenda Fc juzi imeifuna goli 2-1 timu ya Mazombi Fc ya mjini kyela katika mwendelezo wa ligi daraja la tatu mkoani Mbeya.


Mchezo huo uliyo chezwa katika uwanja wa Mwakangale na Mazombi ndiyo walikuwa wenyeji wa mchezo huu wakiwakaribisha wenda Fc katika uwanja wao wa nyumbani.

 Mazombi Fc ndiyo ilikuwa ya kwanza kuliona lango la wapinzani wao katika dakika ya 7 kupitia kwa  mchezaji wake Silvestar Mwapondela.

 goli hilo  ambalo lilidunu kwa dakika 21 baada ya Daniely Ayubu kupanguwa ngome ya wapinzani wao na kufanikiwa kucheka nanyavu dakika ya 26 na dakika ya 61.




Hadi dakika 90 zinamalizika timu ya Mazombi Fc ilikuwa imeshindwa kutamba mbele ya Wenda Fc na kukubali kipigo cha goli 2-1 katika uwanja wao wa nyumbani.

Mwisho





Chapisha Maoni