Na S ophia
Mwaipyana,Mbeya
SANAA ni moja ya kazi ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kuwainua
wasanii kiuchumi na kulitangaza taifa nje ya nchi kupitia sanaa.
"Ngoma za asiri
ni moja ya kazi za kisanaa ambazo zinamtoa mtu kimaisha, zinainua uchumi wananchi
kupitia wasanii, na zinaelimisha na kudumisha mila na desturi za ki
Tanzania" ndivyo anavyosema msanii chipukizi wa nyimbo za asiri Asnah Litimba,
Katika makala ya leo kwa mara ya kwanza na penda kuzungumzia
msanii ambaye amekuwa akitamba katika radio mbali mbali Mkoani Mbeya na nyimbo
za asiri za kabira la wa Yao.
Msanii huyo si mwingine bali anatambulika kwa jina la Asnah
Litimba mkazi wa Masasi Wilayani Mtwala ambaye kwa sasa anaishi jijini Mbeya
akifanya kazi zake za ujasiliamali katika eneo la Sido Mwanjelwa.
Asnah anasema kuwa jambo kuu ambalo limemsukuma kujiingiza katika
sanaa ya muziki wa nyimbo za asiri hasa kabira la wayao ni kutokana na kabira
hilo kutokujulikana sana kwenye nyimbo za asiri.
Anasema kuwa imekuwa ikimuumiza sana kwenye matamasha mengi na
hata kwenye kumbi za starehe, maharusi na kwingineko nyimbo za rugha ya kiyao
hazipigwi na kuonekana kama vile hakuna wasanii.
Msanii huyo alisema nyimbo za asiri zinamafundisho makubwa
ukilinganisha na nyimbo za kizazi kipya ambapo wasanii wengi wamekuwa wakiimba
nyimbo zenye ujumbe wa mapenzi na kuchangia kuharibu maadili kwa vijana nchini.
“Unajua nyimbo za asiri zimebeba ujumbe wa kuelimisha jamii husika
kufuata maadili ambayo yalikuwa yakifanywa na mababu zetu tofauti na nyimbo za
kileo” anasema Asnah.
Aliongeza kuwa kila kabira lina nyimbo zao za asiri na katika
ujumbe mara nyingi nyimbo hizo zinazungumzia mambo yaliyomkuta, walikotoka,
wanakoelekea na nanma ya kuepuka au kujikinga kwa jambo furani.
Alisema kuwa katika albamu yake ambayo ndiyo ya kwanza imebeba
nyimbo (10) na kuzitaja baadhi yake kuwa ni ‘Husi milonga, Mtame pasi, na
Mwanangu mwali.
Aidha alisema kuwa wimbo wa husimilonga unaelezea yaliyomkuta na
ambayo yanaweza kumkuta mtu mwingine wakati wimbo wa Mtame pasi unazungumzia
mabinti kutokumpenda kijana bira kumpeleleza au kuwauliza wazee ili kupata
ushauri.
Pia katika wimbo wake wa Mwanangu mwali unazungumzia namna ya
kumtunza mume ndani ya ndoa ili waweze kuitunza ndoa yao vizuri na kulea watoto
wakiwa wanandoa walioshibana.
Anasema kuwa kipaji chake cha uimbaji alianza toka alipocheza
ngoma ya unyago huko Mtwara na kudai kuwa hadi sasa ananyimbo zaidi ya 100
ambazo ni mchanganyiko wa makabira mengine ambayo amewahi kuishi nao.
Akizungumzia namna watu walivyozipokea nyimbo zake Asnah anasema
kuwa kwa mara ya kwanza alipofanyiwa mahojiano na kituo kimoja cha radio jijini
Mbeya watu wengi walipiga simu wakitaka kujua namna ya kupata CD za nyimbo
zake.
Alisema kuwa watu kutoka mikoa jirani ambako kituo hicho cha radio
kinafika walimpongeza sana kwa kazi yake na kumtaka asirudi nyuma licha ya
kutokuelea lugha ya kiyao.
Akitoa wito kwa wasanii Asnah alisema kuwa ni vyema wasanii wenye
vipaji vyao wajizatiti katika nyimbo za siri kwani nazo nimekuwa zikikonga
nyayo za mashabiki wengi nchini.
Alitoa mfano kwa wasanii kutoka Bostwana wanaojulikana zaidi kama
Makhili khili na kusema kuwa wasanii hao wamejipatia umaalufu ndani na nje ya
nchi ikiwemo Tanzania licha ya watu wengi kutoelewa lugha wanayozungumza.
Msanii huyo aliongeza kuwa nyimbo za asiri zimekuwa zikipendwa na
watu wengi toka nchi mbali mbali siyo tu kwa sababu ya ujumbe bali hata mavazi,
uchezaji wa aina yake na ndiyo maana Makhili khili walijipatia umaalufu
duniani.
Mkoani Mbeya kumekuwepo na ongezeko la wasanii wa nyimbo za asiri
hasa kwa kabira la wasafwa huku msanii ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kwenye
maharusi na kumbi mbali mbali za sherehe ni Awilo Orijino.
Japo wapo wengi wasanii wa kabira la wasafwa ambao wametoa nyimbo
zao ingawa wanafanana vionja vya nyimbo hizo ikiwa ni pamoja na baadhi ya
ujumbe na mistari ya nyimbo pamoja na upigaji wa ghita lakini Awilo amekuwa juu
sana ukilinganisha na wengine.
Pia makbira mengine yameanza kujitokeza katika Mkoa huu ikiwa ni
pamoja na Kabila la wanyakyusa ambapo baadhi yao wamecheza na kuimba ngoma ya
asiri ya Mang’oma na Kapote.
Ngoma ya mang’oma inaendana kabisa na uchezaji wa wasanii wa
Makhili khili lakini tatizo kubwa ni kwamba wanakosa namna ya kujitangaza na
kupata wafadhili ambao wanaweza kuwasaidia ili waweze utoa kitu bora.
Kwa wale ambao wameshafika Mkoani Mbeya na kusikiliza au kuona
nyimbo za siri za Mkoa huo wanavyocheza na kuimba ni dhahili kuwa sanaa ya
muziki kama bongo fleva haiwezi kufua dafu kutokana na ustadi wa uchezaji na
uimbaji wa nyimbo hizo.
Tanzania kuna makabira mengi ambayo yananyimbo zao za asiri lakini
kumekuwepo na ukilitimba kwa baadhi ya makabira kuona aibu au wanajiona kama
kucheza nyimbo za asiri ni ushamba au ni udhalilishaji lakini huku moyoni
wakizipenda.
Tumeona namna makhili khili wanavyovaa na kama ungekuwa
udhalilishaji basi wasingejipatia umaalufu ule na kuweza kutembelea nchi mbali
mbali ndani na nje ya bara la Africa.
Iwapo wasanii wangekuwa pia wanaimba nyimbo zao kwa kutumia pia
mavazi ya asiri hata kama wanaimba nyimbo za bongo fleva bado wangeweza
kujinyakulia sifa nyingi na kujitambulisha kuwa ni watanzania.
Katika makala haya napenda kutoa wito nikiungana msanii Asnah kwa
kusema tudumishe mira zetu kwa kufuata maadili kupitia nyimbo za asiri uchezaji
wa asiri na kadhalika ili tuitukuze Tanzania ndani na nje.
MWISHO
Chapisha Maoni