Na Sophia
Mwaipyana,Mbeya
Mkocha msaidizi aliyekuwa anawaanda wachezaji wa maboresho katika timu yaTaifa Salum Mayanga atangaza majina
ya wachezaji 16 ambao wamechaguliwa kujiunga katika timu ya Taifa.
Kikosi hicho
ambacho kiliweka kambi ya taifa Tukuyu wilayani Rugwe mkoania
Mbeya ambao waliingia na wachezaji 34 kambini
mwezi ulio pita tarehe 22 na kufikia tamati leo.
Akiongea na
wandishi wa habari leo asubuhi katika ukumbi wa Hill view aliwataja wachezaji hao kuwa
ni mlinda mlango Benedict Mlekwa toka (Mara),walinzi wakati wawili Emma Simwanda ( Temeke), Joram Mgeveje (Iringa).
Walinzi wa
pembeni Omari Kindamba (Temeke), Edward Mayunga (Kaskazini Pemba),Shirazy
Sozigwa (Illala) na viungo wa ulinzi ambao ni Yussuf Mlipili (Temeke) na Said
Ally (Mjini Magharibi).
Pia
aliwataja viungo wa ushambuliaji kuwa ni Abubakar Mohamed (Kusini Unguja),
Hashimu Magona (Shinyanga) na viungo wa pembeni ni Omari Nyenje (Mtwara), na Chunga
Zito (Manyara).
Kwaupande wa
safu ya ushambuliaji ni Mohammed
Saidi(Kusini Pemba),Ayubu Lipati (Ilala),Abdurahman Ally (Mjini Magharibi) na
Paul Bundara (Ilala) na wachezaji wa chini ya umri wa miaka 20 (U20), Mbwana
Musa (Tanga) na Bayaga Fabian (Mbeya).
Alisema
kuwawachezaji walio chaguliwa wataondoka
leo kuelekea Dar es salaam kwajili ya kuungana na wachezaji wengi
kwajili ya kunda kikosi cha Taifa.
Naambao
hawaja changuliwa katika kikosi hicho watabaki katika uwangalizi wa shirikisho
la mpira wa miguu Tanzania (TFF).
Chapisha Maoni