Na Sophia
Mwaipyana,Mbeya
Mabigwa wa
ligi ya mkoa wa Mbeya Wenda Fc wamesema wataakikisha kuto uzima moto walio toka nao katika ligi
daraja la tatu hadi ndoto yao ya kushiriki ligi daraja la kwanza msimu ujaoo itakapo timia.
Timu hiyo
ambayo imeshiriki ligi daraja la tatu kwa miaka mitatu mfurulizo bila kufanikiwa
kupata nafasi ya kuuwakilisha mkoa wa Mbeya na kuipata nafasi hiyo mwaka huu waliyo
kuwa wakiingojea kwa hamu miaka nenda mika rudi.
Timu ya
Wenda Fc ambayo maskani yake ni katika mji
mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini nitimu yenye washabiki wengi mkoani
hapa kutokana na timu hiyo kuwa na uwezo
mkubwa wa kulisakata kabumbu na ina wachezaji wanao jituma kama ilivyo timu ya
Mbeya City.
Akiongea na
Championi Ijuma katibu wa Wenda Fc
Muhamed Maurid alisema kuwa nafasi waliyo
kuwa tukiipigania kila siku na kuitamani kuipata sasa wameipata na watahakikisha wanaitumia vizuri hadi kutimiza
malengo yao ya kucheza daraja la kwanza msimu ujao.
“kwasasa
tunajipanga kuanda kikosi kizuri kwajili ya ligi ya kanda ambayo itaanza hivi
karibuni,namshukuru mungu ligi imeisha na wachezaji wote wazima hatuna majerui
hata mmoja hivyo naimani vijana wetu wata jitoa kama walivyo jitoa katika ligi
iliyo pita”
“wadau
wasoka na chama cha mpira mkoa tunaomba wazidi
kutusapoti kama walivyo tusapoti kipindi cha nyuma hadi tukapata mafanikio
ambayo yametufikisha hapa tulipo tunaitaji
kusonga mbele zaidi hadi tuongeze timu katika ligi kuu yani lengo letu
kubwa ni kuwa kama timu ya Mbeya City ilipo sasa”
Timu ya
wenda Fc imeshuka timbani mara tano na haijapoteza mchezo wake hata mmoja hivyo kuwafanya watoke na pointi zote kumi na
tano katika hatua ya sita bora.
Mwisho
Chapisha Maoni